Club History
Rorya United FC ni klabu ya soka iliyoanzishwa rasmi tarehe 1 Juni 2024 na Bw. Peter Owino, Mdau wa maendeleo ya vijana katika michezo Wilaya ya Rorya. Dhumuni kuu la kuanzishwa kwa klabu hii ni kuibua, kukuza, na kuendeleza vipaji vya soka vya vijana katika Wilaya ya Rorya. Tangu kuanzishwa kwake, Rorya United FC imekuwa chachu kubwa ya maendeleo ya michezo kwa kuwapa vijana jukwaa la kuonyesha uwezo wao na kushiriki kikamilifu katika mashindano mbalimbali ya ngazi ya ndani na kikanda.